NAKUPENDA MAMA

NAKUPENDA MAMA

 Huenda ulikuwa ukifuatwa bombani, kanisani na hata sokoni walikufauata sana kifupi ulikuwa  si mpweke karibu kila mahali ulipokuwa.Upweke uliutaka, lakini hukuupata ,japo wengi huepuka upweke lakini kwa upande wako upweke ndicho kitu pekee ndicho ulichoona kuwa na thamani sana maana hukufanikiwa kuupata upweke hata ukiwa usingizini maana ndoto zako nyingi ziliakisi vurugu za wasindikizaji wako.
Ulipojiona mpweke lakini hukuwa mpweke nalo ulilijua hilo, kwa nini usijue maana kila ulipogeuka ghafla basi haikuwa ajabu kukutana na macho si chininya matatu yakiwa yametumbuliwa kukuelekea.  Walipokuja kujua ulipokaa basi wauza mboga , nazi samaki na hata walipokuja kuulizia vyumba vya kupanga waliongezeka japokuwa kwa nyumba ilivyokaa hapakuwa na dalili ya kuwa na chumba cha ziada cha kumweka mpangaji hadi pale baba alipoweka tangazo la kusema hapakuwa na chumba cha kupanga. Baba alipokupa simu kwa kigezo cha kukurahisishia mawasiliano na mama ulifurahi sana kwa kujina umeingia kwenye dunia ya kisasa na ulikuwa ukipata nafasi ya kuwasiliana na mama na baba huko kijini maana walitamani sana kusikia sauti yako kwani licha ya kuwa kabla ulitumia simu za wenyeji wako kuna muda walikuwa wakiona ukiwasumbua bure. Sasa ukawa umejiwekea utaratibu wa kupunguza idadi ya nyanya za kununua sokoni ili upate salio la kuongea  na mama nyumbani, NANI KAMA MAMA?. Kwa kuwa ulikuwa msichana mwenye akili hakuna aliyegundua kuwa kulikuwa na upungufu wa nyanya kwani siku ukipunguza nyanya utazidisha Mchuzi Mix , siku nyingine huweki kitunguu maji ila nyanya zinakuwa za kuzidi nani atajua wenyewe wakija kula washajishibia mishikaki na supu za huko hotelini wanakoenda? Ukajinafasi kila siku unaongea na mama kupitia kwa simu ya jirani wa mama kule kijijini. Siku moja wakati unaongea na mama tena akikusimulia juu ya yule mchumba wako aliyeenda kwao kutaka kukuoa ghafla simu ikaita na kwa hamaki ya kuisaka ndoa na kuwa na nyumba yako ukataka kujua nini kilichofuata kwani ulikuwa umechoka kusindikizwa na wakora wa mjini ulikuwa na kitu ulichotegemea kwa hamaki ukakimbilia ndani na kupapasa jui ya kabati na kuchukua hela uliyoiona asubuhi  wakati unadeki na kwenda kuchua vocha duka la jirani ili umuwahi mama si ulijua simu haikuwa yake na mawasiliano ya kijini kwenu uliyajua wanaweza wasipatikane wiki nzima , mtandao wenyewe wa kusimama pale kwenye kibao cha shule au kule kilimani kwenye kanisa la Romani. Kufika dukani yule kijana wa dukani alidai hakukuwa na vocha labda akurushie salio umlipe nawe kwa haraka ukamtajia namba na kupokea salio na kuwahi nyumbani maharage uliyoyaacha jikoni yasiungue. Kufika nyumbani ulimkuta baba akihangaika kuangalia chini ya makochi, na kabla hujamsalimia akakutupia swali. ”Kuna elfu kumi niliiacha hapa mezani umeiona?” Na wewe kwa kuwa ulijua ilikuwa chini ya kabati na si mezani ukakataa katakata hadi alipotaka kukukagua ukasema ulikuwa na hela uliyoikuta chini ya kabati ambalo ilipita miezi mitatu bila kunyanyuliwa na siku ile kwa kuwa mama alikuwa amesafiri na alikutaka ufanye usafi wa uhakika. Baba alikuja juu na kutaka kukupiga kwa kosa la wizi ukampigia magoti ukimwomba radhi kwa mia tano uliyoitumia na huku ukimpa elfu tisa mia tano zilizobaki lakini hakufanya kitu kingine zaidi ya kupiga simu ile mahali alipopaita polisi na kukufanya umkumbuke mchumba wako , mama yako baba yako na wengine wengi  kwa kifupi jela uliiogopa na uliona itakutenganisha na  watu uliowapenda. Si masikhara  ulisikia sauti ya magurudumu ya gari yakilalamika nje ya nyuma yenu ishara ya kuwa yaliamrishwa  kuacha kuzunguka kabla ya watu watatu waliovalia sare za polisi wakiingia sebuleni kwenu. Kilio kilisikika lakini , hakuna aliyekusikiliza zaidi ya virungu vilivyotua mwilini mwako kwa amri ya baba. Kwa mara ya kwanza ulikiona kile chumba kidogo japokuwa ulikaa masaa mawili tuu ulikiogopa kile chumba kwa kadri kilivyokaa kitesaji uchafu wake yalikuwa mateso tosha. Baba alikuja kuwaomba askari wakuachie wakati ambao yule muuza duka alikuwa ameshakuja na kukupa mia tano ili umlipe baba lakini askari wawili walikuwa hawabandui macho kwako  na hata ulipokuwa ukiondoka na yule baba na kuingia garini kuna aliyekupa kikaratasi bila baba kujua. Ulipofika nyumbani ukajaribu kuomba msamaha huku ukimpa baba ile miatano uliyopewa na muuza duka lakini alikataa akikutuhumu kuiiba ile hela na kukutishia tena kukurudisha polisi. Ukafyata na kusubiri adhabu maana hukuwa na haki mbele ya baba , kwa kifupi alionesha ukali wake haswa na kila ulipokumbuka kituo cha polisi basi ukajikuta ukipoa tuu. Ghafla bila kutegemea ulitazamana na silaha ya moti huku sauti kutoka kwa baba ilikuamrisha kuvua nguo zako kabla ya kuingiliwa kimwili na uliyemwona baba mwema huku akikutishia kukuangamiza endapo ungeleta upinzani wowote na hata alipomaliza haja zake tena sebuleni alikufukuza na kukutishia kukuua endapo ungeropoka popote juu ya alichokufanyia. Masikini zawadi uliyomwahidi kumpa mumeo aliichua asiyestahili tena kwa mabavu huku ukifukuzwa. Hukuwa na ndugu na kitendo kile uliona aibu haswa ukatoak na kwenda kukaa kweny nyuma ya jirani ambayo haikuwa mbali na pale nyumbani ukisikilizia maumivu makali kwani alikuwa amekuharibu haswaa. Ulisikia sauti ya baba akiwasimulia majirani hata yule muuza duka kuwa umemwibia hela na kutoroka lakini pia alikutuhumu kuwa ulikuwa na wanaume na aliwahi kukuonya na baada ya kukufumania zaidi ya mara e kujitokeza ukambishie lakini kila ulipokumbuka ile silaha yake ukaishia kulia, uliwaza ungekuwa na simu basi ungempigia hata mama yako lakini simu nayo alikunyang’anya basi ukawa mtoto wa mtaani. Usiku wa manane huku tumbo lako la chakula likilalamika jaa na lile lingine bado likiuma kwa kitendo ulichofanyiwa ulisikia sauti za watu zilizokiwa zikisogelea nyumba uliokuwa umekaa kisha zikaishia jirani kabisa na ulipokaa na kuwasha kile ambacho hata bila kuelezwa ulijua kuwa ni bangi ambayo moshi wake ulikufanya utoe kikohozi ilichopelekea wale watu wamulike tochi pale ulipokaa na walipokuona kama waliambizana walikusogelea kisha kukufanyia kitendo alichokufanyia baba mchana na safari hii walikuingilia hata kinyume, hadi pale ulipopoteza fahamu. Ulikujankushtuka ukiwa kweny nyumba pembeni yako akiwa yule askari aliyekupa kikaratasi, na akakueleza kuwa wakiwa kwenye doria walisikia harufu ya bangi na walipotaka kuingia kwenye ile nyumba walikimbia na kukuacha na kama bahati ni yeye pekee ndiye aliyepata wazo la kukagua ile nyumba na alipokuona alikuacha kabla ya kurudi baada ya doria na kuja kukupa hifadhi kwake huku akitumia taaluma yake ya udaktari kukutibu. Ulimshukuru sana na  kumwombea kwa Mungu abarikiwe na kumtaka akusaidie nauli uende kwenu, kwa upole akakutaka ubakinpale hadi ukapo pona huku ukiendelea kukaa ndani.Kwa unyonge ukakubali kukaa pale huku akitoka usiku kwenda kazini na kurudi asubuhi hadi ulipopona kabisa lakini ulipomwomba uondoke akakupa la moyoni mwake kuwa alikuwa na pendo la dhati kwako na alitaka muende kijijini kwao kisha kwenu mkambukishane na mpate sakramenti ya ndoa. Ulitamani kupingana na wazo hilo lakini alitumia zaidi ya wiki tatu akikubembeleza huku wema aliokufanyia ukikufanya utamani kumhurumia lakini mchumba wa kijijini akakufanya usite kukubaliana naye hadi alipoamua kwa kinyongo kulipa fadhila zake kwa kumpa pendo lako na haraka haraka haraka  ukapelekea kwao na mlipoamua kwenda kwenu hapo ndipo ulipokelewa kwa dharau na hata ulipomwambia mama yako juu ya madhila uliyopitia alikupa  hadithi na wizi huku ukiambiwa kuwa ulikuwa unegeukia ulimwengu wa wanaume na kitendo cha kwenda na huyo mwanaume basi hawakuwa na wakati wa kusikikiza hoja zako zaidi ya kukufukuza kama mbwa huku wakidai ulikuwa umewaaibisha. Hukuwa na jinsi zaidi ya kurudi na yule askari wako mjini ambako mliamua kuishi kwa baraka za upande mmoja hadi pale ulipogundua kuwa ulikuwa mjamzito. Miezi ikapita hadi ulipojifungua, na hapo ndipo matatizo yalipozidi kwani baada ya kujifungua ukapata ugonjwa wa kutokwa na haja zote bila kujijua hadi mume wako alipokutoroka na kudai kuwa ulijifungua mwezi mmoja kabla ya mwezi aliotarajia kwa mantiki hiyo alidai ulikuwa na ujauzito kabla  ya kukutana na wale vijana kwani aliikuta mipira iliyotumika eneo la tukio na kwa maana hiyo mimba ilikuwa ya baba mwenye nyumba kama utani ulijikut ukifukuzwa kweny nyumba ile siku mbili baada ya kugundua kuwa alikuwa amehama kituo cha kazi na hata ulipojaribu kumpigia simu ilipokelewa na mwanamke ambaye alitishia kukuua kwa kumnyang’anya mume wake kisa hakuwa na uwezo wa kupata mtoto. Hapo ndipo ulipogundua ulitambulishwa wazazi feki na usiku mwingi alidai alikiwa kazini kumbe alikuwa kwa mkewe. Hukuwa na namna zaidi ya kurudi kijijini ambako ulifukuzwa na wazazi wako hadi ulipoamua kwenda kuishi kwa bibi yako amabye naye alitengwa na wazazi wako kwa madai ya uchawi. Nasikitika kusoma barua ya historia yako leo hii nipo darasa la tano, baada ya kuikuta kwenye mabegi ya bibi  yako wakati nahangaika kumtafutia dawa ya kifua kwani anaumwa sana na hapa ameniekeza kuwa fistula ilikuua mama yangu. POLE SANA MAMA YANGU NAKUPENDA NA NITAKUPENDA DAIMA BIBI YAKO NAYE AMEKUFA LEO HII NASHINDWA NITAENDA WAPI UPENDO WENU MKUBWA SANA. Mwisho.

Leave a Reply