SIMULIZI YA KUSIKITISHA KUMHUSU HOUSE GIRL

 House girl mmoja aliajiriwa kufanya kazi katika nyumba ya matajiri sana,. Alifanya kazi kwa kujituma mno na kila mtu alimpenda katika nyumba ile,  kila alipopata mshahara alitumia pesa kidogo na nyingine kuagiza kijijini kwao!  Hakuwahi kuwasahau mama yake na baba yake waliokuwa wazee!    Boss wake alimjaribu kwa kujifanya kadindosha pesa. House girl aliziiokota na jioni akampa bosi wake “mama samahani hii pesa uliidondosha asubuhi, nimekutunzia” mama alifurahi sana. Akampa ile pesa iwe yake,  House girl alifurahi zaidi!   

Mtoto wa bosi alikuwa akisoma nje ya nchi,  akarudi kwaajili ya mapumziko, alikuwa na umri mkubwa kidogo kuliko house girl. Aliitwa John, alikuwa mrefu handsome na mpole sana. Boss alimwambia house girl,  “mwanangu John atarudi leo,  tutaenda kumpokea uwanja wa ndege wote kwahiyo Jiandae!” House girl alifurahi sana,  walienda kumpokea,  John alimtazama House Girl kwa huruma na upendo mwingi,  House girl alimtazama John kwa upendo zaidi. 
 Nyuma ya gari Walikaa John na house girl huku   mama akiendesha gari, ulikmya ulitawala sana katika safari ili ya kurudi nyumbani, house girl alivunja ukimya akaongea na John kwa sauti ya upole na ya chini mno akimueleza hisia zake. “soma John baadae utanioa,  Nakupenda sana John! Nitakuwa mke mwema wa watoto wako! Mungu amekuchagulia mimi niwe wako!” aliongea house girl kwa sauti ya  upole na utulivu huku gari likitembea. John hakujibu kitu house girl akaongezea ………”John unaogopa kwakuwa sijasoma?  Naweza kumlea mwanao vizuri, kupika na kufanya usafi vizuri kuliko hata aliyesoma!  Elewa nakupenda!” 

Maneno haya yalisikiwa na mama wa John akaanza ukorofi wa kumgombeza house girl “eeh wewe huwezi kuolewa na mwanangu aliyesoma huendani nae hata kidogo! Acha kumchanganya mwanangu! Kama utaendelea nitakufukuza kazi” Alisema mama huku akiingiza gari getini.  “nisamhe sitarudia,  usinifukuze ni  mimi pekee nawasaidia wazazi wangu wazee!! Ukinifukuza watakufa kwa kukosa msaada,  nisamehe tafadhali”  aliongea house girl huku akibubujikwa machozi kuashiria alijutia kosa lake!! Hali ile ilimuumiza sana John na kuhisi mapenzi ya kweli toka kwa house girl, John  alibaki kainamisha kichwa bila neno!   Waliingia ndani House Girl alitayrisha chakula Na baadae kumpeleka maji ya kuoga bafuni! John alienda kuoga lakini akiwaza maneno aliyoambiwa na House Girl, “…….mimi naweza kulea,  kutunza kupika na kufanya usafi vizuri kuliko hata waliosoma na nitakuwa mke bora” sauti ya maneno ya House Girl ilijirudia kichwani mwake mwa John kila mara!   
Jioni walikula na kusali kisha kwenda kulala,  ila House Girl na John wakibaki sebuleni kuburudisha macho yao kwa kuangalia Tv.  Bado house girl hakukata tamaa,  alimpenda kweli John, alitumia muda ule kumueleza John hisia zake, ikawa katika kusema mama akatokea chumbani na kuwakuta wakiwa wamekumbatiana pale sebuleni,  aliwakasirikia sana,  kisha akachukua simu na kuondoka, John  na house girl nao pia wakatawanyika kwenda kulala, kichwani mwa John house Girl alikuwa akizunguka tu,  kichwani mwa house Girl ni John alikuwa akisumbua ubongo wake!  “kweli mapenzi yana nguvu kubwa! Sijui itakuwaje ila nampenda huyu Neema House Girl wetu,  mama hamtaki!  Daaa” alijisemea John na kisha kulala.   
Asubuhi mama aliamka na ugomvi,  kusema hata kama mwanae atampenda house girl Neema basi wasingeona kwa kuwa ni familia mbili tofauti, tajiri na masikini.  Pia neema hajui chochote kwa kuwa hajaenda shule,  maneno ya mama yalimkasirisha John na akaoropoka akisema  “mama mimi nampenda Neema nitamuoa hata iweje,  ni mimi nitakayeishi nae sio wewe! Nipo tayri kwa lolote hata kuacha chuo!”  “mwanangu umelewa au? Labda mimi nisiwe mwanao niliyekunyonyesha na hizi chuchu”  huku akishika kifua chake aling’aka mama yule!  Muda wote house Girl alikuwa kapiga magoti kuomba msamaha huku akibubujikwa na machozi mashavuni, John alimshika kisha akamfuta machozi na  kumsimamisha house girl, kitendo kile kilimpa mama hasira akachukua kiti kilichokuwa karibu na kumtupia John kikampata mkononi,  John alikimbia na kufungua geti kisha kwenda  nje na bahati mbaya akagongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi akafa pale pale! Mama alilia sana “mzaha mzaha kamba hukata jiwe” ni kweli John alikufa na kumuachia maumivu makali ya moyo  House Girl,  mama alimchukia na kumlaumu sana house Girl, akamfukuza baada ya mazishi ya mwanae John.  
House Girl Neema hakuwa na pakwenda,  kwa kuwa hakupewa pesa,  aliona bora aende kwenye kaburi la John! Aliomboleza usiku kucha,  mchana alizunguka mjini kutafuta riziki na usiku kurudi kulala akiomboleza kando ya kaburi la John huku mbu wakimbeleza kwa sauti zao na kumnyonya damu mpaka siku arobaini,  akarudi kwao kijijini!!  

Leave a Reply