UKIMPENDA MTU MWAMBIE UKWELI

Siku ya kwanza alimkuta akiwa pekee huku akiwa hana furaha. John alijitahidi kumbeleza Sarah na kumfanya atulie. Alifanya hivyo kwa kuwa ukaribu wake na Sarah ulikuwa hauwez kuficha kitu abadini. Kila mmoja  alijua bayana mabadiliko ya mwenzie. Ndio walikuwa marafiki wakushiba, hakuna kilichowatenga mapacha hawa wasiofanana.

Walitembea pamoja. Walikaa pamoja, wakasoma pamoja. Alichokula John lazima Sarah akionje. Ndio mtindo wao wa kuishi. Siku, wiki, miezi  miaka ikaenda, wakakua, wakanawiri na kupendeza. Minong’ono ikaanza, hawa wawili wana kitu sirini…

John alibeba donge zito kooni. Donge la kuwa na hisia kali kwa Sarah. Yamkini aliona kabisa kuwa Sarah alikuwa mtu wake. Ndio alimpenda kimapenzi kwa muda mrefu! Angetoboaje siri ili Sarah ajue? Piga moyo konde, John alipotezea, maswali lukuki yakatiririka katika bongo yake. Nivunje yai? Niseme? Atanionaje? Itakuwaje!.? Akikataa je? Asiponikubalia? Akikasirika?.. Acha tu tuendelee hivi hivi.. Sarah ni rafiki baki kuwa rafiki, akajisemea huku akibeba mfuko wa daftari na kumkuta Sarah nje akimsubiri..

“unawaza nini J wangu? Hujui kuwa wiki ijayo birthday yangu? Usinifanye nikose furaha!”
Sauti ya Sarah haikufua dafu ya kumtoa John katikati ya pori la mawazo. Alimtizama Sarah macho yakongea nakupenda ila moyo ukamsaliti, ubongo  ukazuia usiseme… Akameza funda la mate kwa fujo..

Birthday
Siku ikafika. John akawa na wakati mgumu ampe zawadi gani. Kila alichofikiri hakuona kama kitakuna moyo wa Sarah. Aliona kila kitu kigumu .. Mwishowe akamua kiume  akapita dukani na kununua ua zuri.. Red rose.. Yes lilikua ua jekundu la ghali  akalihifadhi vema. Alifika nyumbani na kulipulizia perfume yake nzuri. Akalifunga vema na kuelekea kunako pati…

Ndani ya party…
Kila kitu kilifana, tabasumu zilitokeza katika kila uso uliokuwako ndani ya ukumbi. Keki ikaletwa. Wakala vyakula vya kila aina na vinywaji. Muda ukafika Mc akagawa vikadi fulani. John alistuka kupata kadi ikiwa imeandikwa 1. Akiwa anasubiri maelezo mara Mc akang’aka kwa bashasha.
“Namba moja popote ulipo simama na zawadi njoo kwa mtoto aliyezaliwa leo, utampa zawadi na kucheza nae. Atakutambulisha hapa, tafadhali mheshimiwa inuka”

John akasimama kwa uoga, hakuamin, akatembea pole  alifika mbele ya Sarah akapokelewa kwa kumbatio murua lililoambata na busu zito katika paji la uso.. Mwili ukamzizima, moyo ukaagana na mwili kusawiri mapigo yake. Akatoa zawadi akacheza nae ziro distance.. Kitu murua, akatamani aseme, nafsi ikamhukumu kwa maamuzi yake, akausaliti moyo wake.. Akatambulishwa kwa kimombo He is my everything, he is my best friend.. Akarudi kukaa…part ikaisha, siku zikaenda wakashibana kama kumbikumbi..

Miaka ikaisha na miezi kenda.. Mficha maradhi kifo humuumbua akajisemea John.. Bado walikuwa zaidi ya marafiki. Safari hii wakiwa chuo. Ndio walisoma pamoja hadi chuo. Kila mtu akimuangalia mwenzake anaonekana ana kitu cha zaidi ya urafiki. Nani abomoe ukuta huu wa urafiki uliojengwa kwa zege zito na kwa muda wa miaka mingi? Nani angeanza, si John wala Sarah, wote walimeza gundi, wakatulia tuli kama maji mtungini wakisaliti mahitaji ya moyo na nafsi. John aliusulubu moyo wake zaidi hasa alipomkuta Saraha akiwa na mwanaume mwingine, wivu ulipenya na kuganda ndani ya moyo kama barufu.. Akawa muoga, akihofia kupigwa kete na wajanja wa mjini..

Mwaka wa tatu chuo..
Miaka nayo ikasonga, wakazidi kuwa wakubwa. Kila mmoja akificha. Wakahitimu masomo yao kwa ufaulu wa kishindo. Ilikuwa furaha kwao. Siku ya mahafali ikafika. Safari hii John alidhamiria na kuuapisha moyo wake kuwa lazima aseme. Ndio afunguke kuwa ana mapenzi mubashara na mujarabu juu ya Sarah  rafiki wake kipenzi.. Alijiapiza kutotenda kosa tena.. Yes alijisemea: moyo usisaliti nafsi na nasfi isisaliti ubongo na ubongo uamrishe mdomo umwambie Sarah maneno haya sita, NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO… John alifanya mazoezi namna ya kusema akajiridhisha na kuona ya kuwa kila kitu ni chema, akavaa suti akapendeza akaenda kunako mahafali…

Dakika 15….
Sekunde dakika masaa yakasogea,baada ya mahafali kuisha! Wakapiga picha pamoja  na ndugu jamaa na marafiki. Hakuna aliyeficha hisia zake kibindoni. Kila mtu alionesha mapenzi na mbwembwe kede kede.. Naam ilikuwa kama mashindano…

John na dhamira yake huku akitetemeka akamshika mkono Sarah na kumpeleka sehemu bustani ya maua ya kuvutia. Akamkumbatia. Akamsogeza Sarah karibu wakatazamana kwa macho ya huba… Macho yakaongea.. Moyo ukapaa kwa mapigo, dakika tano sasa zilipita, hakuna aliyesema neno. Ila mioyo ikasema kwa kundunda kama watu waliopanda mlimaa kwa kukimbizwa. Joto la mwili likapanda haraka, macho ya Sarah yakajifumba.. Akabakia John mdomo ukitetemeka… Akaufungua sasa dakika ya 10….akauelekeza sikioni mwa Sarah…
NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO… ndio alisema kwa usahihi bila kukwama. Maneno yake sita…

Maneno haya yalisikiwa na kupenya vema katika ngoma za masikio ya Sarah na kumfanya afumbue macho yake. Akamkumbatia zaidi John, akamwangalia vema. Ukimya ukatanda, John akaanza kujawa na woga. Nafsi ikamsuta moyo ukamhukumu, bora ningesubiri, akateta na ubongo wake…

Kimya, kimya kikatanda, kimya dakika ya15,
 Sarah akamgeukia John kimahaba akasema..
NILIKUSUBIRI USEME, I LOVE YOU JOHN!… Maneno yake sita yakaponya msononeko wa John, yakatibu msokoto wa tumbo uliokuja ghafula ndani ya dakika tano, Cameraman akatokea akapiga picha wakiwa wamekumatiana.. Wakaondoka zao wakikokotana kimahaba mara busu, mara hug, mara John akambeba Sarah mpaka chumbani. Aliweza licha ya Sarah kuwa na uzani mkubwa, wabwagana katika samani, kazi ya mikono ya seremala.. Dakika moja mbele .. Camera na taa vikazimwa.. Giza… *************

Morales….
Urafiki uliodumu kwa miaka mingi ni mgumu kuugeuza kuwa uhusiano wa kimapenzi

Ukimpenda mtu sema mapema, kuna wakati ukishampoteza harudi tena

Kukaa kimya kutakufanya upoteze mtu wa ndoto zako…

Ukimpenda sema tu….

Leave a Reply