KISA HIKI KITAKUTOA MACHOZI

Siku ya harusi ikafika. Kila mmoja akawa makini kufuatilia nini kitatokea. Ndugu hasa wa upande wa familia ya kiume kwa akina James wakawa makini wakiwa wanafuatilia mwana wao James atafanya nini baada ya ushauri wa muda mrefu kuwa mtu aliyempenda hakuwa sahihi kwake.

Mawifi na mashemeji wote hawamkubali kabisa mke mtarajiwa wa James binti Ester isipokuwa mtu mmoja tu nae ni mjomba wake James. Huyu alimtia James moyo kuwa harusi ingefanyika na angemuoa mtu wa ndoto zake Ester.
Masaa yakapita, dakika zikaenda bila Ester kutokea kanisani kwenye harusi kutoka huko saloon alikokuwa akipambwa. James woga ukamuingia,  akawaza sana. Akaomba simu yake toka kwa msimamizi wake na kumpigia mkewe mtarajiwa. Muda wote huo wazazi mawifi na wengine walikuwa wakifurahi kuona Ester hatokei wakijua adhima yao ya kumzuia James asimuoe imetia.

Alimpigia simu ikaita bila kupokelewa. Akilli yake ikaanza kuchanganyikiwa, moyo ukajikunyata kwa machungu,  chozi likamlenga mwanaume.
“kapatwa na nini huyu, mbona tulikubaliana leo lazima tufunge ndoa yetu?  Ina maana kaamua kuniacha na kunitia aibu dakika za mwisho. Mungu nipe wepesi katika hili,  natia aibu mie.” alijisemea James baada ya simu kutopokelewa.

Wakati huo muda wa kuanza ibada ulikaribia mno. James alitazama saa yake akaona hakuna muda kabisa. Akapiga simu tena. Safari hii ikapokelewa na bi harusi mtarajiwa Ester na kwa sauti ya huzuni akasema
“James mpenzi wangu Nakupenda sana na moyo wangu uko kwako,  nasikitika sana kukataliwa kwenu. Mwanzoni nilijipa moyo kuwa yataisha,  nikwambie siwezi kuvumila matusi ya mawifi kuwa mimi masikini na sio msomi hivyo siwezi kuwa nawe.

Nimevumilia sana ila nimeshindwa. Siwezi kujiingiza katika ndoa ambayo hakuna hata mmoja aliyeupande wangu. Hakuna hata anayeniona kama mtu. Hata nikiolewa nawe nani atanisaidia?  Nani atapiga nami story!?  Nani atanifariji nikiumwa! James nakupenda sana,  tafadhali chakula na sherehe iliyoandaliwa itakuwa kwaajili ya msiba wangu kwa heri na nakutakia maisha mema hapa duniani.!  Aliongea Ester na kukata simu hima. James alichangayikiwa sana. Alitimua mbio na kuanza safari kwenda kule saloon. Alifika pale akambiwa Ester aliongoza njia kuelekea barabarani kwa sharti la kutaka mtu yeyote asimfuate. James aliacha gari na kuanza  kuongoza barabara, mbele kidogo alimuona mkewe mtarjiwa na kumwita..
“Ester Ester usinikimbie tafadhali…. “
Ester kusikia vile aligeuka huku akikimbia, akajikwaa na kudondoka barabarani na kwa bahati mbaya gari likamgonga akapoteza fahamu pale pale. James akaubeba mwili na kuuweka kando huku akilia sana, watu walikusanyika  Tayari na wazazi nao walifika. Alichukua pete yake mfukoni na kumvika Ester aliyekuwa akivuja damu maeneo ya kichwani
“Ester mke wangu,  nakupenda nakuvika pete hii ishara ya upendo wangu kwako. Iwe ishara ya uaminifu wangu kwako, Katika shida na raha mpaka kifo kitutenge. ” alisema na kumvika Ester pete kidoleni kisha akaunyanyua mwili na kupakia kwenye gari kupeleka hospital. Walipokelewa na kupelekwa moja kwa moja ICU, madaktari wakatumia juhudi na uwezo wao kumtibu ili  kuokoa maisha ya binti Ester.  Masaa matatu baadae, daktari alimwita James na kumweleza kitu
“Mwanangu,  tumejitahidi sana kwa uwezo wetu. Tumefanya kila lililo ndani ya uweo wetu ila  Mungu ni mkuu siku zote. James mwanangu Ester hatunaye tena duniani, pole sana katika hili”
James alilia sana. Akaingia ndani kwenye chumba ulipokuwa mwili wa Ester akaubusu uso wake, akabusu na kidole chenye pete. Akauangalia mwili na  kulia sana.
Akatoka nje na kuanza kutabasamu huku watu wengine wakillia na kumshangaa. Mjomba wake akamuuliza nini maana ya kucheka na kutabasamu wakati wa msiba wa  mtu aliyempenda.. James kwa sauti akaongea
“Kipindi chote tumekataliwa nilikuwa nikilia na kuomboleza ili mtukubalie na kuturuhusu tuoane. Mke wangu Ester alikuwa akilia na kuumia pia. Tumekuwa watu wa kuumia mioyo kwa kukataliwa. Sasa nimeshinda. Nimemvika pete mke wangu nashukuru sana Mungu mwema kwa kulifanikisha hilo.
Mke wangu Ester pumzika kwa amani. Nakupenda sana,  pumzika mateso ya dunia ni mengi, Mungu akipenda tutaona. Nyie wanafiki mwalilia nini? Mwamlilia mtu mliyemkataa?  Ana thamani gani gani kwenu?  Nadhani huu ni muda wa kupongezana na kufanya sherehe ya ushindi ya kuhakikisha mimi siiishi na Ester. Ndio mfurahi, dada zangu mnalilia nini, ni wakati wenu kushangilia ushindi”

alimalizia kuongea na kupanda gari kwenda nyumbani. Msiba ukarudi nyumbani ila James muda wote akawa mtu wa kufurahi tu, hakulia tena. Ester akazikwa,  James akafanya sherehe na hakuoa tena..

Funzo
..Usipende sana kuzuia wapendanao
.. Heshimu maamuzi ya mtu kuhusu kuoa ama kuolewa..
.. Usiwe muuaji wa ndoto na malengo ya wengine,  jiulize hadi sasa umeua ndoa ngapi!? Umefanya wangapi wasioane kwa msimamo usio na maana?
… Kijana ukipenda shikilia msimamo wako nawe utakuwa imara kam jabari.
..Mali, usomi,  pesa na utajiri sio mapenzi,  ila vipo kunogesha mapenzi. Usiegemee mali au usomi katika mahusiano..
tumia sekunde kadhaa kuomba hii sala.
“Ee Mungu mwema mwenye Enzi Kuu, unisaidie nipate hitaji la moyo wangu. Nipate kile ulichonipangia,  nifanikiwe katika ndoa yangu na mahusiano yangu na kuwaambisha watesi wangu.
Ni wewe liyeumba mahusiano unisaidie nipate na kuvikabili vikwazo vyote, kwani kila lililo jema na lenye neema latoka kwako Mungu,  Amina”
Love is beautiful
Love is powerful
Love is invincible and wicked
Marriage is blessing from God ..
Share..
#wants_to_see_you_change_everday..

Leave a Reply