KWANINI ULIKUJA KWA KUSHTUKIZA BABA?

Akiwa bado yuko safarini baba anold akajisemea
“enhee wacha leo nimsurprise wife”

na alitaka afanye hivyo ili kuupima uaminifu wa mkewe baada ya kusikia maneno ya wambea wakisema mkewe huwa anamsaliti jamaa anapokuwa safarini.

Akaanza safari by saa 2 na robo alikuwa ameshafika pale mtaani,akaamua aende kwenye baa moja hivi ili apoteze kidogo muda ili ikifika saa tano aingie ndani kwake ni kama mwendo wa dakika 15 tu kutoka hapo alipokuwepo na nyumbani kwake, kwa wasiotaka kujipa tabu bodaboda ni tsh.1000

Akamchek Whatsap wife akaona yuko online ilipofika saa tatu akapokea text kutoka kwa mkewe

“Mambo dear!
Jamani I miss you mpaka naumwa,tangu asubuhi sijatoka nipo ndani tu nataka nioge nipumzike…….

Mumewe akajibu Ooh pole Darling miss you too….. akamtumia wimbo wa diamond unaosema ” ukilala lala salama kumbatia picha yangu”

Mkewe akamwambia nimeona audio umenitumia nikioga ntaiskiliza my ,akatoka hewani saa hiyo…….

Jamaa ilipofika saa tano kamili akamchek online akaona tangu saa ile aliyosema anaingia kuoga hajaonekana tena online last seen today at 9:17 ilisomeka hivyo.

Jamaa akaanza mdogo mdogo kwenda kwake…..hahaa nahitaji concentration yako hapa.

Alipofika akagonga mlangoni hakuna aliyetoka kuja kumfungulia,akazunguka kwenda kwenye chumba cha mkewe akakuta giza akagonga dirishani wapii!!

Akaita kwa sauti “Jessica!! Jessica! We Jessica! Mama anold! Kukawa kimya……akazunguka chumba cha watoto wake japo alikuwa anajua anawasumbua wamelala

Alikuwa anajua fika mama yao yuko ndani ila labda ako na mwanaume mwingine.

Anold anold! Dogo akaitika alipoamka akauliza nani
Ni Mimi baba yako hebu nenda sebuleni fungia mlango wakati huo watoto wote watatu wakawa wameamka wana furaha kuona baba yao karudi
Lkn baba hana furaha kama walidhani wao.

Dogo akashika kitasa kufungua mlango wa chumba Chao kumbe umefungwa haa!mbona mlango haufunguki wewe joy funguo ikwap

Mbona akati tunalala ilikuwa kwa nje?alijibu joy

Baba tunaomba mwambie mama atufungulie kwa nje maana ametufungia…..what??baba alihamaki kwa hasira akaamua kupiga simu kwa mkewe kama Mara tano inaita tu haipokelewi

Akarudi tena kwenye chumba cha mkewe ili apige akiwa anachungulia ndani na alipopiga simu akaona Mwanga wa simu ipo kitandan MWENYE simu hayupo

Kumbe ametoka yuko nje ndio maana watoto aliwafungia ili wakitoka wasiweze kujua kinachoendelea…..

Mr alikuwa kama amechanganyikiwa omba isikukute hii hali aisee!

Yaani anaenda kufanya upumbavu wake usiku anawafungia watoto wangu?je kama ni nyumba imeshika moto wataokokaje huyu mwanamke muuaji!!

Oky haina shida ndio matokeo ya wanawake tunaokutana nao stend hawa!alijisemea baba anold

Hakujua afanye nini watoto wapo dirishani wanamsubiri dadii alete jibu,dadii hataki wajue kama mama yao hayupo,ni moja ya kiapo ambacho waliweka na mkewe kwamba wakiwa na ugonvi wowote watoto wasijue chochote ili kutokuwaathiri saikoloj yao kimasomo na ktk ukuaji wao kwa ujumla wake.

Alichofanya akaenda akawaambia watafute bisibisi pale chumbani kwao ndani akawaambia cha kufanya pale kwenye kitasa wakafanikiwa kufungua moja kwa moja wakaenda chumbani kwa mama wakakuta hayupo aaaaah sasa mamii ako wapi???

Baba yao akawaita njooni huku mlangoni walipoenda hakuna ambacho wangefanya maana pana mlango wa geti na ndio uliofungwa na kufuri za solex ila mlango wa mbao ulikuwa wazi.

Kwahiyo waliendelea kuongea na baba yao pale mlangoni wakamuamkia……swali la Mtoto wa kike lilikuwa je,sasa mama yuko wapi usiku wote huu baba?

Usijari atakuja muda si mrefu labda anaumwa ameenda kutafuta dawa hospital”aliwajibu baba ili kupotezea……

Baada ya muda ikiwa ni saa sita na nusu za usiku baba akawaambia kalaleni mimi nitakuwa hapa mlangoni namsubiri mama yenu….

watoto wakamkatalia anold akasema haiwezekani labda wakalale hawa ila Mimi siwezi kukuacha peke yako baba…….na wale wengine wakasema hivyo hivyo…….baba akawa hana la kufanya

Akakaa pale mlangoni na watoto wakakaa kwa ndani

Kutokana na uchovu wa safari akawa amepitiwa na kiusingizi…..na watoto pia wadogo wawili wakawa nao wamelala ila anold hakulala kuhakikisha usalama wa baba.

Ikielekea saa saba kama na robo kumbe mama yao akawa anarudi yuko ndani ya gari ya mchepuko anamleta home.

Walipokuwa karibu Jessica akaona kitu cha tofauti pale mlangoni, akamwambia mwanaume azime taa akashuka ili aone kufika akatambua ni mumewe, kule ndani asijue Mtoto wake mkubwa anaona kila kitu.

Akarudi haraka kwenye gari, baba akiwa amezidiwa na usingizi ila alilala mlangoni kabisa kiasi kwamba mlango usingeweza kufunguka na asijue

Anold alishuhudia mama yake mzuri anarudi tena kwenye gari na gari ikaanza kurudi reverse huku taa zikiwa zimezimwa na muungurumo wa gari hausikiki tena ikawa imepotea machoni pa anold ilikuwa kama ni ndoto kwake.

Jessica na yule mwanaume wakapanga njama ili mumewe akaondolewe pale mlangoni awe kama ametekwa,kwa hiyo wakatafutwa vijana kama wanne usiku ile ule wakamtoe pale mlangoni ili yeye arudi na ionekane alikuwepo ndani

“Naomba msimfanye chochote au kumpiga wala kumnyang’anya fedha hela nilizowapa zinatosha na kama hamjaridhika niambieni niwaongeze kuliko kumwibia mume wangu,mtoeni pale kamtelekezeni mahali kwingine halafu Dereva atanirudia na hiyo gari ┬áharaka ili anirudishe nyumbani” alisema Jessica akiwa na huyo mwanaume na hao vijana watekaji…..sawa tutafanya hivyo sister,walijibu

Haraka mchepuko wa Jessica ukaingia ndani na kuvaa koti kubwa na kofia na wale VIJANA wakiwa wamevalia soksi za kuzuia wasitambulikane na wakawa wako tayari kuucheza huu mchezo

Dereva ni mchepuko wa Jessica

Wakati huo anold bado yuko macho anaombea tu kuche haraka ili baba aamke salama pale

Dakika chache wakawa wamefika na gari wakashuka VIJANA wakambeba kama mzoga baba anold,

Babaaaa babaaa babaa anold akawaamsha na wadogo zake wakaungana kumlilia baba yao kutekwa na majambazi ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa hawa watoto……..

wakafika mahali wakamtelekeza baba anold wakarudi haraka kwa mkewe wakamchukua na kumpeleka kwake ile kufika tu akakutana na vilio vya watoto,akagungua akaingia anold akakitoka nje huku analia anakimbilia kwenye njia alikokuwa anapelekwa baba yake babaa babaaa!

Mama akamkimbilia akamdaka akamrudisha ndani nitakutandika wewe unaenda wapi usiku huu!??

Namfuata babaaa niachieee we mama ni muuajiii Mimi sikupendi tenaaaa,mama akamzaba kofi pwa!

Unasemaje?Mimi nimekuzaa unataka laana??

Kwa utaalamu wa mama akafanikiwa kuwatuliza watoto,na wakanyamaza akawakalisha chini akawaambia baba yenu yupo akachukua simu kudanganya kama anampigia “eeh VP umepona?

Aaah pole mume wangu karibu utatukuta maana hata watoto wamegoma kulala mpaka wakuone……….

Akatoa simu sikioni akawaambia laleni mpumzike ila naomba kama mama yenu mnampenda na hamtaki kubaki yatima nisitirini mkiulizwa semeni mama alikuwa ndani humu humu alilala kwenye chumba cha wageni

Akawaahidi kama wangefanya hivyo angewapa zawadi nzuri sana………

Baada ya nusu saa kupita akawa haonekani Mr akapiga simu yake akaona haipatikani.

Akajiuliza wale walimpora simu nini!!

Saa moja ikapita akapata wasiwasi hapo watoto wamekataa kulala ……akamwambia mwanae ngoja nimpigie Dereva tax ili twende police kutoa report

Alipofika wa tax wakaenda kituo cha jirani….

Ile wanafika pale wamkuta police mmoja tu na yule askari akasema hebu kuweni wavumilivu maana askar wameenda kuna tukio la mwizi kuuawa mtaa wa Jirani muda huu huu………

Kumbe aliyeuawa ni mume wa Jessica wakati wale VIJANA walipomtelekeza akawa anarudi kwake akapita karibu na nyumba Fulani mlinzi alipomwona akamwitia watu kwamba ni mwizi,akapigwa hadi akafa………

Dakika kama 10 Jessica akaanza kupokea msg kwenye simu za group watsap wakimpa pole maana wakati anapigwa mumewe wapo waliomtambua kama ni baba anold

Haaa!eti huyo mwizi kauawa mtaa gani?akamuuliza askar.

Askar akasema mtaa wa kona.

Jessica akatoka kidogo pale mapokezi police akampigia mchepuko eti mlimwachia wapi mume wangu? Mtaa wa kona alijibu jamaa short cut

Pale pale akaanza kupaza sauti ya kilio
Askar akatoka vipi wewe unalia nini hapa kumbe mumeo ni mwizi?ndio mavuno yake mama!

Ngoja nifupishe……..uchunguzi ulipokuja kufanyika ikaonekana Jessica ndiye mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya mumewe maana anold alijizira akasema ataongea ukweli mahakamani kuisaidia police na akaeleza mkasa nzima na Jessica akamtaja mchepuko wake kuwa walishirikiana na wale watekaji wakakamatwa na kila mmoja anatumikia kifungo cha miaka 30 jera……….

Anold sasa hivi ni mtu mzima amesomea sheria ni mwanasheria mzuri sana!

Tatizo pekee alilonalo amekataa kuoa haamini kamwe mwanamke,ila anasema;

Siku moja akitoka mama yake atamuuliza maswali matano:-

1.kwanini alikuwa akimsaliti baba?
2.hakukuwa na mbinu nyingine ya kufanya zaidi ya mbinu ya kumteka baba?
3.kitu gani alikikosa kwa baba ambacho kilimfanya amsaliti?
4.atanisaidiaje mimi na ugonjwa nilionao wa kutokupenda na kutokusamehe?
5.nini faida ya yote aliyokuwa akimfanyia baba?

Katikati ya msiba wa baba yake aking’ang’ania jeneza anold alilia alisema:-
Baba kwanini ulikuja kwa surprise?
Baba kwanini hukwenda kulala guest?
Baba mbona umetuacha hatujakukumbatia
Nachukia mlango wa geti nachukia funguo ya mlango
Namchukia aliyenizaa ni afadhari kama nisingezaliwa
Eeh mwenyezi Mungu ulinileta duniani ili nione maumivu haya?mimiiii mimiiii ntaenda wapi mimiiii na wadogo zangu hawa!huyu mtoto aliliza sana watu msibani……..

Yapo yanawatokea watu ila ni siri zao za ndani.
Tuwe waaminifu ktk ndoa zetu.

MWISHO

Leave a Reply