NISAMEHE MKE WANGU

James aliondoka asubuhi akiwa na hasira kutokana na ugomvi na mke wake aliyekuwa mjamzito.  Licha ya utajiri, mali pesa na magari waliyomiliki lakini ndoa yao haikuwa na furaha kabisa.  Irene mkewe James alichoka kabisa. Alitamani kungekuwa na mapumziko basi angepumzika ila haingekuwa hivyo kwani bado alitakiwa kuwalea watoto wake mapacha na ujauzito miezi 7 nao Ulishika hatamu.
Hii yote ilitokana na tabia ya mumewe James kubadilika mno toka wafunge ndoa.  Zamani za uchumba James alikuwa kijana mpole mcha Mungu na Mkarimu mno. Alionesha upendo muda wote. Sasa alibadilika, alikuwa mkali na msaliti mno.  Irene alijua fika hayo baada ya kuambiwa na kushuhudia mipira ya kiume Ikiwa imetumika ndani ya nguo za mumewe James pindi azifuapo!! 

Irene alijipa muda na kumuombea Mumewe abadilike alee watoto wake,  ijapo alishaambiwa mwanaume akiingia kwenye ndoa hubadilika. Aliamini ipo siku mumewe atatulia na Kuleta heshima ya ndoa na furaha kama awali. Akiwa bado katika kuwaza pasi na habari mara mumewe alirudi toka kazini muda usio wa kawaida. Irene alimuuliza kulikoni. Majibu aliyopata yalikata maini yake mithili ya kisu chenye ncha kali.
“Huwezi kuniuliza uliza kwani mie mtoto?  Nilichofuata hapa hakikuhusu,  we tulia endelea kuwepo hapa.  Mambo yangu hayakuhusu kabisa ikiwezekana leo sirudi kabisa!l” aliongea James kwa saiti ya kejeli na kumfanya Irene atokwe machozi mbele zake,  hakujali kabisa,  aliingia parking na kuchukua Gari jingine na kuondoka. Irene alijiuliza sana kwani asubuhi James aliondoka na gari sasa lingine la nini? 
Nyumbani  Irene alilia na kupiga goti akimuomba Mungu amusaidie majaribu anayopitia na kumrudisha mumewe. Kutokana na maumivu tumbo lilianza kumuuma ghafla. Hakuwa na msada na magari ya kutembelea yote alichukua mumewe…. Alimpigia simu mumewe bila mafanikio kwan kila alipopiga haikupokelewa,  alikata tamaa kabisa. Akamua kuomba msaada wa teksi ili afike hospital…. 
James alipeleka gari kwa hawala yake Diana aliyekuwa kamuomba atembelee gari hilo la kifahari kwa siku hiyo. Baada ya kukabidhiwa gari hilo aina ya BMW alianza kupiga misele town kwa masifa mengi mno. James akiwa  ofisini alikaa kwenye kiti chake na kutafakari kwa muda maisha anayoishi,  moyo ulimuuma akaingiwa na hofu fulani,  akajua kuwa anachofanya sio kizuri akajisemea potelea mbali. 
Wakati akiwa bado anaumia nafsini kwa kumkatili mke aliyempenda na kumletea mapacha, alistushwa na mlio wa simu!  Alijua ni mkewe tena. Alitupia jicho kwenye screen ya simu na kukutana na jina la Diana. Haraka alipokea simu ile.. 
“Halo baby kuna vinyago viwili vimekwaruza gari langu, Nipo hapa maeneo ya Sinza Mori! Naviambia vilipe havitaki kabisa,  sasa njoo uwaoneshe kwamba wewe ndiwe mwananaume. Wanakiteksi tena cha zamani na limwanamke libaya, sijui lina ujauzito maana… Fanya fasta hubby! ” alimaliza Diana kwa msonyo mkali na kumfanya James ainuke haraka kitini na kuvaa koti lake alilokuwa kaliegeaha nyuma ya kiti cahake tayri kwenda eneo la tukio. 
Akiwa anafunga mlango wa ofisi yake na kuwaaga wenzake kuwa kuna dharula,  mara simu iliita mfukoni.  Alichukua haraka akijua ni Diana tena. La hasha,  hakuwa huyo bali jina lilisomeka “Lovely Wife!”  laaah!  Alifonya James na kubinya batani ya kupokelea simu kwa hasira akasema:
“Unataka nini wewe? Una shida gani na nini kinakusumbua? “
aliongea James kwa ukali.. 

“Mume wangu toka uondoke nimeumwa tumbo ghafla mno. Nimepiga simu hujapokea, nikakodi teksi na sasa tumepatwa na matatizo kidogo,  naomba uje mume nipo katika shida mume! Gari yetu imekwaruzana na BMW hapa na mwenye nalo hataki kabisa tuelewane please nakuomba mie mkeo uje!  Niko chini ya miguu yako! “” aliongea kwa sauti ya upole mno Irene na kujibiwa na mumewe
“Sitaweza kuja huko mie. Muelewane tu. Nitakuja kukuona  hospital baadae nikimaliza mizunguko yangu sawa! ” aliongea James na kukata simu haraka na kupanda gari. Upesi gia ilipachikwa na kwa mwendo wa kasi gari liliendeshwa na James Kuelekea Sinza Mori kama alivyoambiwa na Diana. 
Baada ya dakika tano alikuwa karibu na Sinza Mori. Kulikuwa na msongamano mkubwa magari tofauti na ilivyozoeleka. James alimwita mtu mmoja mtembea  kwa miguu na kumuuliza kulikoni hadi magari yakasimama. Aliambiwa ni ugomvi kati ya watu wawili,  ila dada ni mkorofi hataki kusamehe wenzake na wanamgonjwa. James alipaki gari pembeni akashuka na kutembea haraka akienda mbele. 
Tahamaki aliona gari lake aina ya BMW na mwanamke akigombezana na watu. Alisonga zaidi na kubaini kuwa aliyekuwa akigombana pale ni Diana.  Alitizama pale kwenye ugomvi ambapo wenye busara na hekima walikuwa wakijaribu kupatanisha bila mafanikio na kufanikiwa kumuona mwanamke akilia kwa uchungu sana. Hatua kadhaa  alizipiga mbele na alijionea vema,  aliyekuwa akilia alikuwa Mkewe Irene!
Akiwa  katika mshangao,  Diana akamuona James na kuanza kujidai mbele ya mkusanyiko ule wa watu:

“Mniache,  mume wangu kafika sasa nataka niwaone nyie kina nana mfyuuuuu ” aliongea kwa tambo huku akimwangalia James aliyekuwa kaduwaa tu.  Maneno yale yalisikiwa na watu na Irene pia aliyekuwa akilia kwa kwikwi na kumfanya afute chozi ili amuone huyo mume aombe msamaha aendelee na safari ya hospital.
Hakuamini macho yake kumuona mumewe akiwa pale, alibaki kaduwaa tu. Watu walikaa kimya wakimuangalia James. Kwa takribani dakika 5 na sekunde kadhaa James alikaa kimya kama mtu aliyepooza.
Kisha akafungua kinywa na kusema
“Mke wangu Nisamehe sana. Nimekukosea sana, nimekuwa nikifanya vitu vya ajabu kama vile mimi mtoto. Siwezi kumsingizia shetani! Kweli nimekosa mno” wakati huo Diana alijichekesha huku akitembea pole pole kumwelekea James.

“Mimi nilijawa tu na tamaa. Ni muda sasa nimekutesa mke wangu najutia sana. Leo nilikaa nikafikiri nikaona kabisa nasitahili adhabu nzito toka kwako na kwa wanangu kwa tabia yangu mbovu. Tafadhali mke NISAMEHE!” watu walikuwa kimya mno. Hata Diana sasa alikuwa mpole na mdogo zaidi ya pilitoni. 
“Diana,  nashukuru sana kwa kumtukana mke wangu. Nadhani ulikuwa hujui. Huyo ni mke wangu anayenipikia na kunitunza. Hata kama nilimtesa kwaajili yako bado alinifunika na kunifanya nionekane mtu!  Anahakikisha nimevaa vema,  nmeenda kazini na niko sawa. Nimekuwa nawe kipindi chote mke alijua ila akavumilia. Diana nipe funguo na uondoke mbele ya macho yangu” watu walishangaa mtu aliyejidai mmiliki wa mume na BMW akitoa jasho jingi makwapani hadi unyayoni. Diana alitembea kwa uoga na kumkabidhi James funguo za BMW na kuondoka kwa aibu. 
“Mke wangu NISAMEHE sana. Njoo nikuwahishe hospital tumuokoe mtoto wetu huyo” aliongea James baada ya kukabidhiwa funguo na Diana. 
“NIMEKUSAMEHE mume! Nitakuombea kwa Mungu akusamehe pia! NAKUPENDA mume wangu” aliongea Irene kwa sauti ya majonzi kisha akajikokota taratibu huku watu wakimtambua sasa mke halali wa James. Irene alimfikia James na kumkumbatia kisha James akamnyanyua na Kumpandisha kwnye BMW. Alimlipa dereva taksi na kumuomba msamaha kwa usumbufu.  Akapaki gari lile lingine pale na kuanza safari ya kumpeleka mkewe Hospital.
Toka hapo James alibadilika na Kuwa Mume bora!! Kesho waliruhusiwa na James akampikia mkewe chakula kitamu cha kumuomba msamaha yeye na wanaye,  ikawa furaha kubwa ndani ya ndoa na familia yao.! 

*******        ********* *********
Kama nakuona vile wewe unayejisifu kuwa mumeo kumbe wenye mume wametulia tuli.
kama  nakuona vile unavyolinga na gari la watu wakati huna haata baiskeli. Dada acha kupoteza muda,  tafuta mume wakoKamwe usijidanganye kuwa utamnyang’anya mwenzako mume! Mwanaume tuliza ball kati,  angalia familia. Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake sio mwanaume. Wanawake wanajua hili… Usiwe mchoyo share

Leave a Reply