FURAHA ILIYOPOTEA

Helena alisoma kwa shida sana kutokana na familia yake kuwa ya kipato cha chini, daima alimuomba Mwenyezi Mungu amfungulie milango akafanikiwa kupata wafadhili wakamsomesha hadi chuo kikuu, akamaliza akamuomba Mwenyezi Mungu kazi pia akapata, alimuomba Mwenyezi Mungu pia akafanikiwa kupata mchumba akampeleka kwao wakapata baraka za wazazi hatimaye wakaoana. Kimbembe kikaanza baada ya wiki, miezi na hatimaye miaka kukatika pasipo kupata mtoto, ndugu wa mumewe walicharuka na kuwa mbogo. Walibadilika na kumtukana hadharani kuwa amekua kuku wa broiler kwa kijana wao. Hii ni kutokana na ukweli kuwa baada ya vipimo ilionekana Helena ndio mwenye matatizo katika mirija ya uzazi hivyo uwezekano wake wa kuzaa ulikua mdogo mno. Helena alilia sana alijuta kufika hatua aliyofikia, alimlilia Mwenyezi Mungu akisema, “Ee! Mola, kwa nini umenisahau, nadhalilika kiasi hiki? Naomba kusudi lako katika maisha yangu litimie”.
Helena aliumia sana alitamani hata kujiua maana jamii yote inayomzunguka ilikua ikimuita tasa, mgumba n. k, alitokwa machozi kila alipokumbuka alipotoka mda aliotumia shuleni kusoma kupata kazi hadi kuolewa, kila aliyejaribu kumfariji alihisi anamsanifu. Mume wake siku moja alipotoka kazini ijumaa jion aliongozana na rafiki yake (Aitwae Emanuel Msoka ambaye ndio admin wa Online News Tz)
na kumueleza tatizo la mkewe (Helena), Mr. Jacob alimwambia sasa wanafikiria kwenda kwa waganga sumbawanga ikibidi hata nigeria ikishindikana basi akasema wako tayari bora wajiue wafe tu maana aibu na masengenyo yamezidi na katu hawezi kumuacha mkewe, rafiki yule aliguswa sana maana mme wa Helena alisimulia akitokwa machozi na kusema kibaya zaidi ndugu zake wanamfosi amuache ila hayuko tayari maana anampenda sana mke wake.
Rafiki yule alimtuliza kisha akamwambia,” Mr. Jacob poleni sana hakika ndoa yenu ipo katika kipindi kigumu, najua mmepitia hospitali nyingi, waganga na sehemu mbali mbali imeshindikana, huenda viongozi wa dini uliokutana nao pia kupata dua na maombi hawajasimama kwa Mwenyezi Mungu ndio maana mnateseka tu, ila nakushauri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndio aliyekupa vyote kwa makusudi yake, kila mlalapo na muamkapo MSHUKURUNI MWENYEZI MUNGU NA KUMUOMBA AWAFUTE MACHOZI hakika mtaupata muujiza wake mda sio mrefu maana kwake hakuna linaloshindikana “
Mume wa Helena alirudi nyumbani siku ile kwa furaha akamsimulia mkewe wazo hilo jipya, wakaweka utaratibu wa kumuomba Mwenyezi Mungu kabla na baada ya kulala, kabla na baada ya kushiriki tendo la ndoa.
Baada ya miezi mitano wakiendelea na utaratibu wao wa kusali na kuomba huku wakitoa sadaka kwa makundi maalum ikiwemo yatima na wajane ambao wengi wao walifurahi mno baada ya kupokea na kuwaombea Mwenyezi Mungu awabariki na kuwatimizia haja za mioyo yao, hatimaye haja ya mioyo yao ambayo ilikua ni kupata mtoto ILITIMIA.
Helena alipata ujauzito madaktari walistaajabu wakasema Mr. Jacob huenda ana nguvu za kiume kali mno maana kwa namna mirija ya uzazi ya mkewe ilivyokua imepinda na kuziba ingekua vigumu mno kupata mimba, ila Mr. Jacob aliwajibu, “NI KWA NEEMA YA MUNGU TU”. Hatimaye Helena alifanikiwa kujifungua watoto mapacha.
Furaha ilirejea upya katika ndoa ya Helena na mumewe (Mr. Jacob), Helena alifurahi sana kila akiwatazama mapacha wake hutabasamu na kumshukuru Mungu kwa kusema, “HAKIKA SASA NAIONA FURAHA YANGU ILIYOPOTEA”
Funzo
Huenda Mwenyezi Mungu amekubariki katika mambo mengi mno ila jambo moja linataka kukufanya umsahau au umsaliti Mungu .
Huenda Mwenyezi Mungu amekujalia umesoma sana ila ajira hamna kila ukiomba unakosa hadi rafiki zako ambao walifeli wanakucheka.
Huenda Mwenyezi Mungu amekujalia uzuri, sura na tabia njema ila huolewi hadi majirani na marafiki wanakuita bibi unaezeekea nyumbani.
Huenda Mwenyezi Mungu amekujalia umepata kazi, elimu, pesa ila ndoa inakutoa jasho mkeo /mmeo hakamatiki, unalia na kujuta kuzaliwa.
Kama taarifa ya Helena kujifungua mapacha ilivyokua mbaya kwa adui zake ndivyo itakavyokua kwa adui zako wanaochekelea taabu unazopitia siku ya leo watakaposikia uliyopitia sasa yamekwisha, imebaki story.

Leave a Reply