MKE VS HAWARA

Ni asubuhi moja hivi jamaa anaondoka kwenda kazini anamuaga mkewe.
“Mimi pia nitatoka mchana ntaenda mahali charger ya laptop yangu imekufa ntaenda kununua”alijibu huyo mkewe.
“Ok basi tutawasiliana my love” alijibu mume.
mlinzi anafungua geti jamaa anatoka na gari yake…..
Mwanaume ni mfanya biashara wa magari na ana yard yake ya magari.
Mchana akaja ofisini hawara yake akamwomba gari moja afike mahali jamaa bila hiyana akampatia ufunguo wa gari moja wapo zinazouzwa, dada akandoka na gari.
Alipofika mahali fulani mtaa fulani akawa amepaki vibaya gari yake na ikapita gari nyingine ikamkwangua na yakwake ndiyo iliumia zaidi.
pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa mkorofi, akashuka kwa kiburi ndani ya gari akaanza kumgombeza mwenzie , aaaaaaah kumbe ni yule dada mwenye mume ko hapo ni kwamba hawara anagombana na mwenye mali ila hawajuani maskini!…..achana na bongo move hii ilikuwa ni zaidi ya picha la kikorea.
lakini huyu mama alikuwa na hekima maana pamoja na kwamba alionewa kiasi fulani lakini alianza kumwomba msamaha huyo dada….. Dada akaanza kutukana matusi mazito akitaka alipwe….
Basi kutokana na hiyo shida wakawa wameshawakusanya watu wakawa wamejaa wakishuhudia hiyo move itaishaje japo wengine walijaribu kutoa ushauri ili wayamalize kiundugu na wengi walionekana wako upande wa yule mama. Walikerwa na kelele za yule mdada ambaye alionekana sio mwelewa.
Basi huyu mama akaamua kumpigia simu mumewe.
Hellow baby, nimepata tatizo kidogo hapa
“Tatizo gani? Aliuliza huyo mumewe
“Nilikuwa napita mahali {mtaa akautaja} nikawa nimekwangua gari ya mtu alikuwa amepaki vibaya gari yake halafu anataka kulipwa, naomba uje basi”
“Aah mimi niko meeting kidogo mahali , jaribu kuona kama utamalizana nae au mpigie simu fundi aje”. Jamaa alimjibu mke wake halafu akakata simu.
Kusema ukweli mkewe alijiskia vibaya sana akijiuliza “inamaana kazi yake ni ya muhimu kuliko tatizo langu?
Na je, kama angeskia nimekufa kwa ajari ingekuwaje?
Hivi mme wangu ananipenda kweli?
Kwa upole na kwa unyonge akamwendea huyo dada akitaka waelewane, lakini huyo dada hakuthubutu hata kumwangalia!
Akajibu, enhee huyo kinyago mwenzio uliekuwa unampigia simu amesemaje!!?
Hahahaahaaaa ngoja nikuonyeshe aina ya wanaume wanaojari , wanaojua maana ya mapenzi! akaweka simu sikioni kwa madaha akitaka akampigia mumewe
hello darling! Naomba uje mara moja…….. Kuna kinyago mmoja amenikwangua , sijui gari yenyewe ameazimwa na hajui nashindwa kumuelewa yaani!!
Jamaa dakika 10 zilikuwa ni nyingi akaenda na pikipiki eneo la tukio akawa amefika akaona umati wa watu umezinguka hizo gari
akaamua ajipenyeze, ile kufika akashangaa kuona gari zote ni za kwake, kasoro ni kwamba mmoja ni mke wake halali aliyemwambia niko bize, na mwingine ni hawara yake!!
Whaaaaat!!? Akamtazama mkewe usoni akaona analia
Akamtazama hawara akaona anasogea ili amueleze vile ilivyotokea akasema no no nooo!! Give me the key nipe ufunguo!……..
Watu wanaangalia lakini hawajui kinachoendelea,
mama na baba wanajua kinachoendelea,
hawara hajui kinachoendelea ila anamshangaa jamaa kabadirika na kuwa mkali ghafla
Akamsogelea mkewe na kumkumbutia na kumfuta machozi akamwamwomba msamaha akisema “nisamehe mke wangu, wewe ndiye mama wa watoto wangu, hawa tunawapitia tu kwa upumbavu wetu, ila ndio chanzo kikubwa cha ndoa zetu kuvunjika.
najua umeumia, nimetii sauti ya huyu wakati wewe nilikukatalia, nisamehe plz sintarudia huu upuzi! na kukuonyesha kama sintarudia huu upumbavu, ingia ndani ya gari ile aliyokuwa nayo huyu mpuzi wewe nipe ufunguo wa gari yako naendesha mimi, wewe ndiye mmiliki na mwangalizi wa mali zangu.
Akaenda kufungua mlango wa gari akatanguliza mguu mmoja, halafu akamgeukia hawara kumpa vipande vyake,
Samahani shantel kwa kutokukutambuli
sha.
Unakumbuka nilikwambia mimi nina mke? Anhaa basi ndio huyu, hakuna uamuzi mwingine wowote ambao ningeufanya zaidi ya huu.
Asante kwa kumtukana mke wangu kwa kumwita kinyago, sasa hapa ndio itajulikana kati ya wewe na mke wangu nani kinyago, nani kaazima gari, nani limbukeni……. Bye bye!! Akaingia ndani ya gari akampa ishara mkewe atangulie mbele kwa usalama zaidi yeye afuate nyuma….wakaacha simulizi nzito eneo lile.

Leave a Reply