UPENDO WANGU UMENIPA UKILEMA

Ni mwaka mmoja tu umepita tangu mimi Aisha nifunge ndoa na Mume wangu Ally.Mwanzo maisha yalikuwa mazuri kiasi kwamba nilitamani hata tusizeheke wala kufa lakini ghafla mwenzangu alianza kubadilika.Nilimchunguza nikajua kuwa tayari ananisaliti na ana mwanamke mwingine nje. Nilichukulia tu kama kawaida ya wanaume kutokuridhika lakini nilichojivunia ni kuwa mimi ndie mke halali na mwenye pete kidoleni hao wengine ni wapita njia na wala hata siku moja hawataweza kusogea kwenye mji wangu zaidi ya kuishia kuchezewa tu na kuachwa,Pamoja na hayo yote japo niliwaza sana na kuwa na hofu endapo sasa mme wangu ataniletea magonjwa ya zinaa itakuwaje. Ila niliishia kujipa moyo na kutupilia mbali mawazo kama yale na zaidi ya hapo sikutaka hata kumuuliza mme wangu chochote kuhusu huyo mwanamke alienae nje,Niliishia tu kusema mimi ni mke halali na nina mamlaka na Ally wangu.
Sikujua kama ukimya ule na upendo ule kwa mume wangu baadae utakuwa mateso makubwa sana. Siku moja nikiwa nimekaa sitting room naangalia Tv niliona sms imeingia kwenye simu yangu na namba ni ngeni.Niliifungua Sms ile na kukuta ujumbe unaosema”Achana na Mume wako vinginevyo tutakuachanisha”.Nilijiuliza sana hii namba ni ya wapi na inatoka wapi sikupata jibu.Lakini moja kwa moja wazo likaja huyu ni mchepuko wa mume wangu yule ambae nilikuta sms zake kwenye simu ya mume wangu.Sikutaka hata kujibizana nae kwa sababu niliona ni ujinga na wala sikutaka hata kumuuliza chochote mume wangu japo sms ilikuwa ni ya vitisho.Niliona tu kuwa huyu mdada hana jipya kakosa la kufanya zaidi ya umalaya wake na anataka tu kunigombanisha na mme wangu.Sikutaka hata siku mmoja mimi na mume wangu tuje tugombane au nimuwekee kinyongo chochote.Nilichokuwa napenda ni kumuona mume wangu anafuraha siku zote hilo tu lilinifanya nijisikie raha na kujiona kuwa nina mume nimpendae hivyo sikutaka kujua au kusikia ni wanawake wangapi wanatoka na mume wangu na anawahonga kiasi gani haya yote sikuyataka. Hivyo niliamua kuifuta ile sms wala nisibaki nayo kwenye simu.Kufanya hivyo kumbe ndio nilikuwa nazidi kujichimbia zaidi kaburi.
SIKU moja wakati natoka saloon kutengeneza nywele zangu mida ya saa moja inaelekea saa mbili usiku.Nilikuwa kwenye kiuchochoro napita ili nikatokezee barabara kubwa kisha kupanda pikipiki nielekee nyumbani. Nikiwa kwenye kale ka uchochoro ghafla wadada watatu walijitokeza na kunizuia njiani. Kabla sijafanya chochote mmoja wao aliniziba mdomo kisha kunivuta pembeni.Nikiendelea kutahayaruki mwingine alinishika kwa nguvu zaidi nisiweze kufanya chochote kisha yule kiongozi wao akaniambia”Si nilikutumia sms uachane na mumeo ukaniona mimi fala.Anaefaa kuolewa na mumeo sio wewe ni mimi hapa sasa leo tutakufundisha”Nikiwa siwezi kuongea chochote kutokana na kuzibwa mdomo yule dada alitoa kitu kama chupa yenye maji maji.Nilitamani kupiga kelele lakini ilishindikana.Nilitamani niombe msamaha lakini ilishindikana zaidi nilibaki kutoa macho kuangalia nini anataka afanye.Nikiwa nimetoa macho yangu nilishangaa kuona anaitikisa ile chupa kama mtu anaechanganya dawa kabla ya kunywa. Mara ghafla bila huruma mwanamke yule alinipulizia dawa ile machoni mwangu ambapo muda huo nilikuwa nimeyatoa zaidi kwa ajili ya kushuhudia tukio.Niliyafumba kwa maumivu makali sana ya ile dawa aliyonipulizia na ghafla macho yangu yakaanza kuuma.Nilijalibu kufumbua angalau nione kitu ama hakika huo ndio ulikuwa mwisho wangu wa kuona DUNIA
Nilisikia sauti ya yule mwanamke akisema”Na bado leteni nyundo”.Moja kwa moja nikajua sasa wananimalizia uhai wangu.Nyundo kali ilitua katika mguu wangu wa kulia na kusababisha maumivu makali sana katika mwili wangu.Nilipiga kelele ya kuungurumia ndani kwa ndani kwenye tumbo pasipo hata kutoa sauti kutokana na Maumivu makali niliyoyapata.Kabla hata maumivu ya mguu huo hayajapoa mara……..
…..Nyundo ilinyanyuliwa na kunivunja mguu wa pili.Hapo maumivu yalizidi zaidi na kujikuta naanza kulia ijapokuwa tayari ni kipofu.”Hii ndio dawa yake”.Walisema wale wanawake huku wakicheka kisha kuniachia na kunikimbia.Nilianza kulia damu nyingi zilinitoka miguuni nilipiga kelele hatimae nikazimia. Nilikuja kupata fahamu na kujikuta nipo mazingira ya tofauti.Nilijaribu kufumbua macho lakini sikuona kitu.Nilisikia kelele za hapa na pale na hatimae nilisikia sauti ya mama ikisema”Jamani mwanangu amezinduka”.Mara pia nilisikia sauti ya mume wangu ikinitakia pole huku kwa mbaali mama alianza kulia.Niliuliza niko wapi hapa,Mama alichukua jukumu la kunielezea.”Uliokotwa na wasamalia wema na kukufikisha hapa kisha wakatumia simu yako kumpigia mme wako kuwa upo hospitarini leo ni siku ya pili tangu uletwe hapa ulikuwa umezimia mwanangu nilijua nimeshakupoteza.”Mama alianza kulia kwa kwikwi kitendo kilichosababisha na mimi nianze kulia”Ona mwanangu dunia vile mbaya wamekuvunja miguu na pia wamekuharibu macho sijui umewakosea nini mwanangu”.Maneno haya ya mama yalinifanya nizidi kulia zaidi hasa baada ya kusikia nimekuwa kilema wa milele.
Yote haya yamesababishwa na hawala wa mume wangu.Nilijisemea moyoni,sikutaka kusema chochote zaidi ya kukaa kimya na wao kuamini kuwa ni vibaka ndio walionitendea haya. Nilikaa hospitali takribani wiki mbili nikihudumiwa na hatimae nililuhusiwa. Nilipotoka hospitarini moja kwa moja nilifikia kwa mume wangu lakini cha ajabu nilikaa siku ya kwanza na ilipofika siku ya pili Mume wangu aliniambia niende nyumbani na Mama nikakae kule mpaka nitakapokaa vizuri na miguu itakapoungana vizuri nitarudi.Aliniambia kuwa pale hamna mtu wa kusema nikae nae na kuniangalia hivyo bora niende nyumbami mama yupo.Alinipa maneno ya faraja kuwa japo kuwa nimepoteza macho lakini mimi bado ntabaki kuwa mke wake hivyo nitakapopona vizuri nitarejea nyumbani na atafanya mpango zaidi ikiwezekana tusafiri nje ya nnchi nikatibiwe macho. Nilikubariana na nikasafiri mpaka mkoani kwetu na mama na wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi miwili.
ZILIPITA kama wiki mbili hivi tangu niludi kwetu.Siku moja usiku sikuamini baada ya mume wangu kunipigia cm na kuniambia”Mimi na wewe basi tena,Siwezi kuwa na mke kilema taraka zitakufuata huko huko”.Kisha simu ikakata.Nilishindwa kuitafuta namba nimpigie tena kwa sababu ya upofu wangu.nilibaki nalia tu.Nilimuelezea mama yangu hayo maneno nae akanitia maneno ya faraja na kunifanya nipunguze kulia”Mwanangu angalia vilema wote vile wanavyotengwa na jamii wewe sio wa kwanza,Maadam nipo mimi mwanao nitakulea mwanangu Mungu atakusaidia tu utapona zaidi mshukuru Mungu kwa yote wewe pia sio wa kwanza kuachika ipo siku Mungu atasikia kilio chako utapona na kusimama na kuona tena mtumaini Mungu.” Hakika maneno haya yalikuwa ya faraja sana kwangu.Siku hazikupita na kweli niliachika kwa Mume wangu nilianza maisha ya kukaa nyumbani na mama yangu huku nikijuta ni bora toka mwanzo ningefungua kesi,Ni bora toka mwanzo nisingempenda mume wangu kiasi hiki,Ni bora ningeusema ukweli wote yaliyonikuta.Upendo wangu ka kukaa kimya kwangu kumeniponza.Nashukuru Mungu nilijifungua salama na nina Mtoto japo nae nasikia kaoa tena nadhani atakuwa yule mwanamke alienitendea mabaya haya.Sifa na shukrani naludisha kwa mola japo sioni. Lakini napenda kuacha ujumbe huu kwa jamii na kuwauliza wanaume.KWANINI HAMTOSHEKAGI??
ASANTENI……

Leave a Reply