UMEPOTEZA NDOTO ZANGU

Akiwa anaendesha gari Mr.Lee alitekwa na mawazo sana, Biashara,familia sambamba na majukumu mengine ndiyo yaliyoifanya akili yake iwe bize kuchanganua hayo huku ikisahau kama yupo barabarani akiendesha gari. Kufumba na kufumbua macho yake yalishindwa kuushawishi ubongo wake kuwa yamemuona mutu akikatisha barabara katika zebra kisha kuchukua maamuzi, badala yake alijikuta anashituka ghafla na kubana breki bila hata kukwepesha gari. Mara alifumba macho huku meno akiwa ameyang’ata, kwa mbali ngome za masikio yake yalisikia sauti ya kishindo kidogo cha kugonga kitu, huku sauti ile ikiwa imesindikizwa na sauti nyororo ila yenye uhalisia wa maumivu ndani yake. Ghafla ufahamu ulimrejea na kugundua amemgonga mtu.alifungua mrango haraka na kutoka kwenda kumtazama. Masikini Mr. Lee wala hakuamini macho yake baada ya kumwona dada mrembo aliyekuwa akifanya mazoezi kwa kuendesha baiskeli amelala chini huku damu nyingi zikimtoka eneo la kichwani. Alimfata haraka na kuanza kumuinua huku akimsemesha, alifanya hayo huku akitaza kila upande ili aombe msaada kwa watu wamsaidie kumuinua amkimbize hospitali , huwenda akaokoa maisha yake. Alipoona watu wapo mbali kidogo aliamua ajaribu kumuinua yeye mwenyewe. Alipoanza kumuinua yule mwanamke mrembo alimshika mkono Mr. Lee na kujitahidi kuzungumza. Mr. Lee alipoona mwanamke yule anataka kuzungumza alichutama kando huku wakiwa wameshikana mikono na kumsikiliza kisha mwanamke aliyazungumza haya “umepoteza ndoto zangu,naondoka na jeraha moyoni mwangu. Nilisoma kwa shida sana kutokana na hali duni ya wazazi wangu, sikukata tamaa kwakuwa nilikuwa nina ndoto maishani mwangu.tazama upepoteza ndoto zangu. Wazazi wangu walinisomesha kwa kujinyima huku wakiamini ipo siku nitakuwa msaada kwao, maombezi yao kila siku juu yangu ili nifanikiwe na nije kuwasaidia siamini kama kweli yameishia hapa. Umepoteza ndoto zangu. Nina wiki moja tu tangu nilipoajiriwa kwenye kampuni kubwa na kusaini mshahara mnono, sijaonja hata harufu ya mshahara huo wala matunda ya elimu yangu niliyoipigania hadi kufikia level ya Masters. Sijui wazazi wangu, ndugu zangu, na marafiki zangu watalipokeaje hili kwakuwa nilikuwa ni mtu mwenye matumaini makubwa ya kuja kuwasaidia siku za usoni, umepoteza nguvukazi ya Taifa maana serikali ilikuwa ikinitanbua kutokana na elimu yangu. Tazama umepoteza ndoto zangu wala siwezi kupona tena.ni uzembe tu wala siyo kingine maana hii ni zebra. Hujanipoteza mimi pekee bali umetupoteza wawili, nina mtoto tumboni, sijui mume wangu ambaye nimetoka kufunga naye ndoa miezi mitatu iliyopita ataipokeaje taarifa hii. Hata hivyo huwenda siyo kosa lako, huwenda siku zangu zimetimia, haustahili kulaumiwa wala kuadhibiwa juu ya hili. Ila mwanangu, mwanangu, mwanangu…..” Alipokwisha kuzungumza hayo dada yule alikata roho huku akiwa ameshikana mkono na Mr. Lee. UMEPOTEZA NDOTO ZANGU ni maneno ambayo aliyatilia mkazo sana ila haikuwa na jinsi, hatima ya maisha yake iliishia pale. Mr. Lee hakuamini kitendo kile, alijikuta anapiga magoni anaangua kilio kizito huku akiwa amejiinamia. Aliijutia sana nafsi yake, akiwa bado amejiinamia huku akilia alitamani dada yule apone kisha ampe hata nusu ya utajiri wake. Mr. Lee alipoinua uso na kumtazama dada yule kwa mara nyingine huku akilia, alishangaa kuona watu wamejaa wamemzunguka wakiwemo polisi. Walimshika wakamfunga pingu na kuongoza kwenye gari la polisi. Kabla hajapanda kwenye gari aligeuka na kumtazama dada yule, alishuhudia mwili wake umechukuliwa kwenye machera ukielekezwa kupakiwa kwenye gari la wagonjwa. Aliutazama mwili ule hadi unapakiwa na kufungwa mlango “UMEPOTEZA NDOTO ZANGU” ni neon la mwisho yalilojirudia kichwani mwake kisha akajinenea moyoni “NASTAHILI KUHUKUMIWA” na kuingia ndani ya gari.
MWISHO
****************
FUNZO:
Kwa upande wangu ingawa simulizi hiyo amezungumziwa dereva wa gari ambaye alikatisha maisha ya msichana mwenye ndoto za kufika mbali, ila wapo wengine ambao si madereva na wanatenda hayo. Mfano wanaume kuwapa ujauzito wanawake na kushindwa kuendelea na masomo kisha kuwatelekeza wakilea wenyewe, wafanyakazi kuwasababishia wafanyakazi wenzao kufukuzwa kazi kutokana na wivu, kulogana kisa mtu anafanya vitu vya maendeleo, na vingine vingi. Siku zote kumfanyia mtu kitu ambacho hastahili kufanyiwa au kitu kile ukifanyiwa wewe hupendezwi nacho ni dhahili unatenda unyama ambao mwanadamu hastahili kutendewa. Yatupasa tuwe makini kwa kila jambo,tutafakari kwa kina kabla ya kutenda. uzembe wako mdogo sana unaweza ukamgarimu mwenzio kwakiasi kikubwa na kumpotezea dira kabisa kwa kitu alichokuwa anakitumainia.

Leave a Reply