FUNDI GEREJI

SAA NANE USHEI hivi mchana, Mudi alikuwa gereji anakofanyia kazi. Sinza Afrika Sana. Gereji si gereji hata. Isipokuwa ni eneo ambalo mafundi makenika wameamua kuwa wanafanyia shughuli zao za hapa na pale. Wanatengeneza magari yenye mushikeri. Mjini kuna mengi. Eneo hilo lina taswira mbili zinazotofautiana. Ukipita mchana, magari mabovu yanatengenezwa. Vijana kadhaa waliovalia maovaroli yaliyofubaishwa kwa oili chafu, huhangaishana huku na kule. Spana zikiwa mikononi. Huku wengine, wakiwa uvunguni mwa magari wakiendelea kufunga ama kufungua kifaa hiki ama kile. Hayo yakiendelea, zogo mtindo mmoja. Pita sasa usiku. Pahala ambapo mchana uliiona gereji huku vijana wa kiume wakihangaishana na spana, inageuka kuwa gereji nyingine. Ila hii ya usiku, wala si vijana wa kiume tena wakihangaishana na spana. Sasa ni vijana wa kike. Wao, hawahangaishani

CHOCOLATE ILOYOUA MTOTO WANGU

Yapata mida ya mchana jua likiwa limetoa ndimi zake kuiramba ramba dunia hapa jijini dar hali ya joto ilikua juu sana. Nikiwa ni daktari katika hospitali ya Temeke wodi namba tatu ya wanaume, siku hiyo nilichelewa kufanya "AROUND" ya kupitia wagonjwa wa wodi ile mpaka mida ya mchana bado nilikua sijamaliza zoezil lile. Nilikuja kukatishwa baada ya kufika kwa mgonjwa aliyelala kitanda moja wapo pale wodini nilipomkuta anabubujikwa na machozi yasiyokawaida shuka aliyolalia ilikua imeloa tepetepe.Niliwajua vema wagonjwa waliokua wodi ile lakini yule aliyekua analia alikua mgeni kulazwa huku katundikiwa dripu Wajibu wangu ulikua ni kujua Analia nini huwenda anasikia maumivu au kuzidiwa, sikuwa na budi kumfata "shikamoo baba" nilimsalia kwani alionesha kanizidi umri zaidi ya miaka kumi na

USISAHAU ULIPOTOKA

Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari. Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini. Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki nayeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri. Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini. Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu

HOUSEGIRL

"Kwanini umenifanyia hivi mke wangu, pamoja na kukupenda kote kule lakini umenifanyia mambo ya ajabu sana...." Rajabu aliongea kwa sauti ndogo yenye kuonesha maumivu makuu ndani yake."Stop! Ishia hapohapo mjaa laana wewe, kwanza nani mkeo, labda useme nilikuwa hawala yako, cheo ambacho kwa sasa sikipendi hata kukisikia. Eti unanipenda, hivi unavyoniangalia mimi nina hadhi ya kupendwa na wewe, achana na mimi mwanaume suruali wewe!" Hanifa alisema kwa jazba huku akiwa ameshika kiuno chake, misuli ya shingo ikiwa imemtoka, ama hakika alikuwa amedhamiria."Hanifa, leo hii mimi nimekuwa mwanaume suruali, sawa sikatai kweli kwa sasa mimi ni mwanaume suruali, tena unaweza kuniita hata mwanaume boksa kabisa, sina kitu kwa sasa lakini ni wewe ndiye...." Rajabu hakumalizia alichotaka kusema."We we we! Koma kabisa,

KILIO CHA VALENTINE

(Aibu Kusimulia)‘’Ni aibu kufikiria, itakuwa kusimulia?’’ Sauti ya Latifa ilisikika kupitia simu, ni dhahili alikuwa akilia.‘’Pole sana ndugu yangu lakini aibu hadi simuni, tena ukitumia jila la kificho?’’Nilijaribu kumpooza kwa kuingiza utani kwenye maongezi yetu kumbe nilikuwa kama nimechochea kilio chake.Akakohoa na kuonesha kapaliwa mate, kisha akatulia na kuendelea kuongea safari hii sauti yake ilionesha huzuni na uchungu aliokuwa nao achana na aibu aliyokuwa nayo tangu awali.‘’Jina feki ni kwako Michael, kwa Mungu na wahusika tunaolijua tukio hili ni jina halisi hata ningejiita kiumbe wa kutoka sayari ya mbali kuna watu duniani, Mungu na malaika zake wanalijua hili’’Alimeza mate na kutulia kwa muda (nadhani alikuwa akijaribu kufuta machozi yaliyokuwa hayakomi) kamasi zilisikika zikirudishwa zilikotoka.Kisha akaendelea.‘’Michael ni aibu, aibu ambayo kama

UMEPOTEZA NDOTO ZANGU

Akiwa anaendesha gari Mr.Lee alitekwa na mawazo sana, Biashara,familia sambamba na majukumu mengine ndiyo yaliyoifanya akili yake iwe bize kuchanganua hayo huku ikisahau kama yupo barabarani akiendesha gari. Kufumba na kufumbua macho yake yalishindwa kuushawishi ubongo wake kuwa yamemuona mutu akikatisha barabara katika zebra kisha kuchukua maamuzi, badala yake alijikuta anashituka ghafla na kubana breki bila hata kukwepesha gari. Mara alifumba macho huku meno akiwa ameyang’ata, kwa mbali ngome za masikio yake yalisikia sauti ya kishindo kidogo cha kugonga kitu, huku sauti ile ikiwa imesindikizwa na sauti nyororo ila yenye uhalisia wa maumivu ndani yake. Ghafla ufahamu ulimrejea na kugundua amemgonga mtu.alifungua mrango haraka na kutoka kwenda kumtazama. Masikini Mr. Lee wala hakuamini macho yake baada ya kumwona dada mrembo

TAFAKARI NJIA ZAKO

Mchungaji mmoja alijibadili na kuwa omba omba katika viunga vya kanisa alilokuwa akitarajia kutangazwa jumapili hiyo kama ni mchungaji mpya wa kanisa lile akitokea mji mwingine. Alitembea kuzunguka lile kanisa akiwa amevaa nguo kukuuu zilizochanika chanika huku akipishana na watu waliokuwa wakiingia kanisani. Ni watu watatu tu ndio waliomsalimia. Wengine wote hawakutaka hata kumuangalia mara mbili, walipitiliza moja kwa moja na kuingia kanisani. Aliwaomba watu msaada wa chakula au hela ya kula hakuna hata mmoja aliyempa chochote. Akaenda katika malango ya kanisa na kukaa katika ngazi akaweka chombo chake ili aguswae atoe msaada lakini hakuna hata mmoja alietoa hata senti moja. Akainuka na kwenda mbele kabisa ya kanisa, akakaa benchi la kwanza kabisa, mzee wa kanisa akamwambia aondoke pale na

MCHEPUKO SIO DILI

" Baada ya kuishi kwa muda mrefu ndoa iliyokua imejaa amani furaha na mafanikio huku tukishirikiana bega kwa bega na mke wangu kipenzi hakika sikuwahi kufikiria ipo siku familia yangu itakuja kusambaratika, inauma sana , leo nimeona nishuhudie yaliyonisibu  hivyo naamini ushuhuda wangu huu utakua funzo kubwa mno kwa wengi. Iko hivi, Nilikuwa ninafuraha kufikisha miaka 35 ya Ndoa yangu mimi na mke wangu, kwa pamoja tulipitia mengi milima na mabonde. Mwenyezi Mungu alitubariki watoto wazuri na wenye akili, watatu wa kiume na mmoja wa kike.Wote kwa sasa wana ndoa zao, na wana kazi zao nzuri tu, shukrani kwa mke wangu aliyewalea kwa muda mwingi zaidi na kuwakuza katika maadili ya dini yetu.Nilistaafu katika utumishi wa umma, ambako nilihudumu takribani miaka

DAKIKA CHACHE KABLA YA KIFO CHANGU

Nayaandika haya huku mtiririko wa matukio mengi yaliyotokea baina yangu na wewe yakigonga kichwa changu. Nakumbuka wakati ambapo tukiwa pale chuo kikuu cha Dar es Salam, wakati ambapo tukiwa ni vijana wenye matarajio makubwa sana siku za usoni.Ukiachilia mbali ukata, ucheleweshwaji wa fedha za kujikimu sanjari na lapsha za kila siku tukiwa pale Mlimani, hayo hayakukufanya uangukie kwa mapedeshee kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wanafunzi wengine wa kike.Urembo wako hukuugeuza kuwa mradi wa kujipatia fedha. Ni wewe uliyenifundisha kuwa penzi halinunuliwi kwa fedha, ulisema mtu anaweza kununua mwili kwa thamani ya pesa vile awezavyo lakini siyo moyo wa mtu, wakati wote ulisisitiza kuwa unahitaji penzi la kweli kutoka kwangu, ukaongeza kuwa furaha na faraja ndiyo mambo muhimu kwenye maisha yako.Tangu

FURAHA ILIYOPOTEA

Helena alisoma kwa shida sana kutokana na familia yake kuwa ya kipato cha chini, daima alimuomba Mwenyezi Mungu amfungulie milango akafanikiwa kupata wafadhili wakamsomesha hadi chuo kikuu, akamaliza akamuomba Mwenyezi Mungu kazi pia akapata, alimuomba Mwenyezi Mungu pia akafanikiwa kupata mchumba akampeleka kwao wakapata baraka za wazazi hatimaye wakaoana. Kimbembe kikaanza baada ya wiki, miezi na hatimaye miaka kukatika pasipo kupata mtoto, ndugu wa mumewe walicharuka na kuwa mbogo. Walibadilika na kumtukana hadharani kuwa amekua kuku wa broiler kwa kijana wao. Hii ni kutokana na ukweli kuwa baada ya vipimo ilionekana Helena ndio mwenye matatizo katika mirija ya uzazi hivyo uwezekano wake wa kuzaa ulikua mdogo mno. Helena alilia sana alijuta kufika hatua aliyofikia, alimlilia Mwenyezi Mungu akisema, "Ee! Mola,