HUYU NDIYE MAMA WA KUIGWA

Rehema alifika nyumbani mbio mbio na kumkuta mama yake aliyekua migombani akipalilia viazi vyake, "Mamaaa, hodi hodi humu nyumbani" aliita Rehema, "Naaaam, karibu nan jirani?" aliuliza mama yake Rehema, "Ni mimi mwanao Rehema mama" alijibu Rehema. Mama aliacha shughuli zake shamban na kurudi haraka, alimkuta mwanawe kaja nyumbani kutoka mjini anakoishi na mmewe ila cha ajabu kaja kidharura katika hali inayoonesha hayupo sawa yani atokako hali si shwari."Haya nieleze mwanangu nini kimekusibu waja mbio mbio kwangu kwa dharura kama kasuku"aliuliza mama Rehema," Dah ndoa imenishinda mama nimechoka mwanaume hashikiki nimeamua kurudi nimechoka visa mimi bora nikae nyumbani mama "alieleza Rehema. Mama yake alimuangalia namna alivyokua kavaa kikahaba akamwambia," Mwanangu kwa nini unanidhalilisha hivi, mmeo alivokuja kukuoa kijijini alikuchukua ukiwa na

OMBA OMBA

Ilikuwa ni takribani miaka miwili imepita toka aonane na familia yake kwa sababu za ulinzi wa amani nchi mbali mbali duniani.Sio tu mke..bali hata watoto wake walikuwa na furaha ya ajbu kumwona baba....Howard na samweli hawakubanduka kwa baba yao..wakimparamia paramia muda wote..Ilikupata Muda mzuri na familia yake, Kamanda George alijadiliana na mkewe Jane kwamba waende mapumzikoni mbali na Nyumban.Usiku ulikuwa mrefu sana kwa familia hii..wote walitamani kukuche waanze safari.Mziki mzuri toka ndani ya speaker znye ubora ziliwaburudisha njiani...stori utani...vinywaji laini vilishushwa taratibuuu...furaha iliyoje ndani ya Mercedes benz new model.Ghafla kukawa na mtikisiko mkubwa garini..vinywaji vikamwagika na wengine kujigonga..kutokana na brake ya ghafla...Mzee George alishindwa kujizuia kusimama ghafla baada ya kijana aliyemwona kwa mbali akichechemea kusogea barabarani ghafla akilia kwa sauti

TANGA USIKU WA MANANE

Mimi si mshirikina na mambo ya imani za jadi ziambatanazo na mambo ya kichawi kwangu ni kama hadithi za Hisopo na visa vya sungura na fisi. Katika pitapita yangu hapa yote hapa Bongo hata hivyo, nimekutana na watu wengi ambao wanaapa kwa majina ya wazazi wao na wengine hata wanaapia vifo cha watoto wao kuwa ati wamewahi kuona mambo ya kichawi au kushuhudia maluweluwe ya wataalam wa jadi. Hata nilipoenda masomoni kuanza kidato cha kwanza kule Ufipani watu walinishangaa na kuniasa niombe uhamisho kwani kule Sumbawanga “kwa wachawi ndio wenyewe”. Maneno yao hayakunitisha wala kunikatisha tama. Nilienda na bila hofu yoyote ile nilianza na hatimaye kumaliza masomo ya sekondari pale Kaengesa Seminari. Kwa muda wote huo sikupata kujikuta nimechanjwa usiku

UPENDO WANGU UMENIPA UKILEMA

Ni mwaka mmoja tu umepita tangu mimi Aisha nifunge ndoa na Mume wangu Ally.Mwanzo maisha yalikuwa mazuri kiasi kwamba nilitamani hata tusizeheke wala kufa lakini ghafla mwenzangu alianza kubadilika.Nilimchunguza nikajua kuwa tayari ananisaliti na ana mwanamke mwingine nje. Nilichukulia tu kama kawaida ya wanaume kutokuridhika lakini nilichojivunia ni kuwa mimi ndie mke halali na mwenye pete kidoleni hao wengine ni wapita njia na wala hata siku moja hawataweza kusogea kwenye mji wangu zaidi ya kuishia kuchezewa tu na kuachwa,Pamoja na hayo yote japo niliwaza sana na kuwa na hofu endapo sasa mme wangu ataniletea magonjwa ya zinaa itakuwaje. Ila niliishia kujipa moyo na kutupilia mbali mawazo kama yale na zaidi ya hapo sikutaka hata kumuuliza mme wangu chochote kuhusu huyo

MKE VS HAWARA

Ni asubuhi moja hivi jamaa anaondoka kwenda kazini anamuaga mkewe."Mimi pia nitatoka mchana ntaenda mahali charger ya laptop yangu imekufa ntaenda kununua"alijibu huyo mkewe."Ok basi tutawasiliana my love" alijibu mume.mlinzi anafungua geti jamaa anatoka na gari yake.....Mwanaume ni mfanya biashara wa magari na ana yard yake ya magari.Mchana akaja ofisini hawara yake akamwomba gari moja afike mahali jamaa bila hiyana akampatia ufunguo wa gari moja wapo zinazouzwa, dada akandoka na gari.Alipofika mahali fulani mtaa fulani akawa amepaki vibaya gari yake na ikapita gari nyingine ikamkwangua na yakwake ndiyo iliumia zaidi.pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa mkorofi, akashuka kwa kiburi ndani ya gari akaanza kumgombeza mwenzie , aaaaaaah kumbe ni yule dada mwenye mume ko hapo ni kwamba hawara anagombana na

SUMU YA KUMUUA MUME

Binti alifika kwa mama yake kumlalamikia kuhusu ndoa yake. Malalamiko yake yalikuwa kama ifuatavyo: BINTI: Mama, mume wangu amenishinda. Ninataka kumua lakini nakosa ujasiri wa kufanya hivyo, unaweza kunisaidia tafadhali? MAMA: Ndiyo binti yangu, ninaweza. Lakini kuna tatizo dogo utatakiwa kulishughulikia kwanza. Itakubidi uanze kutengeneza mazingira na hali ya amani kati yako na mumeo ili kwamba watu wasikutilie shaka kwamba wewe ndiye umehusika na kifo chake. Utatakiwa kuwa mwema sana, mpole na umhudumie kwa moyo wote. Uwe romantic, uwe unamshukuru sana, uwe mwenye subira, na mnyenyekevu kwake. Mchukulie kama mwanao badala ya kumchukulia kama mkubwa mwenzio au raia wako… usiwe mbinafsi, uwe mnyoofu, msikilize sana, msafishe, mnawishe, usimsumbue au kumponda. Mwanangu, nina uhakika kwamba unaweza kuyafanya hayo, huna sababu ya

NILIKATAA UCHUNGAJI NIKAWA MKUU WA WACHAWI

TAKRIBANI wiki tatu nilikuwa nafuatilia mkasa wa dada Easter Deo. Hakika mkasa huo ulinigusa sana nami nikashawishika kusimulia yaliyonikuta katika maisha yangu.Naamini kuwa kuna baadhi ya watu hawakuamini mkasa wa dada Easter kama ni wa kweli ama ulikuwa ni wa kutunga. Ninachoamini ni hiki, uchungu wa maumivu ya ugonjwa ama majeraha yoyote huwa anayasikia mhusika lakini si mtu mwingine. Kwa jina naitwa Steven Frances Soso, ni mwenyeji wa Morogoro Wilaya ya Ifakara. Nimezaliwa katika familia ya wacha Mungu. Baba yangu mzee Frances Kasela Soso ni Mchungaji wa Kanisa la Living Word Pentecost lililopo Ifakara. Nilikuwa na hali ya kuwa naumwa mara kwa mara. Pamoja na kwamba baba yangu ni mchungaji, binafsi sikukubaliana na masuala ya ulokole kwani niliona kama ni shida kwangu.Baba yangu

JERAHA LA MOYO

Jana usiku niliamka mida ya saa nane, na kama kawaida yangu, nikalia sana. Ni ajabu kwa mwanaume kulia, lakini kwangu imekuwa kitu cha kawaida sana. Nadhani ninapolia huwa najihisi nafuu kiasi, na kwa namna fulani napunguza uchungu ulio ndani yangu. Nimekuwa nikifanya hivyo kwa muda wa mwaka mzima sasa, lakini usiku wa jana ulikuwa tofauti kidogo. Baada ya kulia sana, niliamua kwamba huu ndio utakuwa mwisho. Mwaka 2007 tarehe kama ya jana nilikutana na binti mmoja nikiwa masomoni Arusha. Huyu binti ni mmang’ati kwa kabila, ana urefu wa wastani, rangi ya ngozi nyeupe inayofanana mwili mzima, yaani si kama rangi za mabinti wa siku hizi za kuchanganya na kutafutiza. Ni mzuri mno kwa sura, kama unavyojua wadada wengi wa mkoa huo.

MAPENZI… MCHEZO WA HATARI

Inawezekana utasema nilikuwa fala na mwingine akasema kwamba nilikuwa mjanja. Kuna msichana namkumbuka kichwani mwangu, jina lake aliitwa Amina Saidi. Alikuwa msichana mrembo kwa sura, umbo na vitu vingine ambavyo msichana wa kisasa alitakiwa kuwa navyo. Mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa katika Chuo cha Ustawi kilichokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Nakumbuka alikuwa akisubiri daladala kituoni, magari yalikuwa shida mno kwani mataa ya pale Sayansi yalizuia kabisa magari kupita. Nilipomuona, sikutaka kuchelewa, nikalisogeza gari na kushusha kioo, nikaanza kumwangalia. Kwanza sikuamini kama Tanzania tulikuwa na mrembo kama alivyokuwa Amina, kila nilipomwangalia, alinivutia mno. Nikapiga honi, Amina akayageuza macho yake na kuniangalia, nikamuita kwa kutumia mkono wangu, akaja na kuinamia dirisha la gari langu. Alikuwa msichana mpole mno ambaye mara

DADA LAKINI UNAJUA BABA ALINIBAKA?

Nilishasema siwezi tena kuajiri mfanyakazi wa ndani, tabia za mume wangu kutembea na wafanyakazi wa ndani zilinilazimisha hata kuacha kazi ili nisiwe na sababu ya kuajiri mfanyakazi na kufanya kila kitu mwenyewe.Niliamua kuwa Mama wa nyumbani ili tu kulinda familia yangu, watoto wangu wawili wadogo wa mwisho niliwalea mimi mwenyewe, hii ni baada ya mume wangu kutembea na wafanyakazi wa ndani watano, wawili akiwapa mimba na kutoa na mmoja kumzalisha kabisa.Nilijua mume wangu hawezi kuacha hiyo tabia kwani kila siku aliomba msamaha na nikimsamehe alirudia tena. Lakini nikiwa nimeshamaliza kabisa kuzaa, Mungu akinijaalia watoto wane nilijua nimemaliza, ghafla nilijistukia nina ujauzito.Mwanzoni sikujua kwani nilipokosa siku zangu nilijua kuwa ni uzee umekaribia, miaka 45, mtoto wangu wa mwisho akiwa na miaka